Kuanzia tarehe 6 hadi 8 Oktoba, Kongamano la Viongozi wa Kimkakati wa Dunia la 2024 limefanyika mjini Guadalajara nchini Mexico. Kwa kufuata mwaliko wa Baraza la Shule za Shahada ya Uzamili na Uzamivu la Marekani, Mkuu wa Jumuiya ya Elimu ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu ya China Bw. Yang Wei ameongoza ujumbe kuhudhuria kongamano hilo. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian ameshiriki na kutoa ...
Tarehe 11 Oktoba, Spika wa Cyprus Bi. Annita Demetriou ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha BFSU na kutoa hotuba. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amemkaribisha. Baada ya kutoa hotuba, Bi. Demetriou amezungumza na kujibu maswali ya walimu na wanafunzi wa BFSU.
Kuanzia tarehe 22 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua ameongoza ujumbe kutembelea Marekani, Kuba na Panama. Amehudhuria kwenye Kongamalo la Wakuu wa Vyuo Vikuu “10+10” vya China na Marekani na kutoa hotuba. Wajumbe hawa pia wametembelea vyuo vikuu vya Marekani vikiwemo Chuo Kikuu cha Northwestern, Chuo Kikuu cha Chicago, Chuo Kikuu cha Stony ...
Tarehe 21 Septemba, sherehe ya kuzindua “Kiti cha Msomi wa Utafiti wa Malaysia cha Sultani Ibrahim” imefanyika. Mfalme wa Malaysia Ibrahim Sultan Iskandar ametia sahihi ya kuidhinisha. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Juu ya Malaysia Prof. Azlinda Azman, Balozi wa Malaysia nchini China Bw. Norman Muhamad, Waziri wa Usafiri wa Malaysia Bw. Loke Siew Fook na ...
Tarehe 20 Septemba, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Cologne, Mwenyekiti wa Kituo cha Mawasiliano ya Kiutafiti cha Ujerumani Bw. Joybrato Mukherjee ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua amekutana na mgeni huyo na msafara wake. Wamezungumzia utafiti, mawasiliano ya walimu na wanafunzi na masuala mengine.
Tarehe 15 Septemba, Chuo Kikuu cha BFSU kimeanzisha kozi ya Kitetum kwa mara ya kwanza nchini China. Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Zhao Gang, Mwambata wa Elimu wa Ubalozi wa Timor-Leste nchini China Bw. Rogério Paulo Chaves wamehudhuria ufunguzi wa darasa na kutoa hotuba kabla ya kipindi kuanza.
Tarehe 7 Septemba, Naibu Waziri wa Elimu wa Kenya Bi. Beatrice Muganda Inyangala na msafara wake wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua na Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian wamekutana na wageni na kuzungumzia mawasiliano ya utamaduni na ushirikiano wa elimu. Prof. Wang Dinghua ameeleza matunda mapya ya BFSU katika usimamizi wa elimu ya dunia, maende...
Tarehe 5 Septemba, Kongamano la Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika lenye mada ya “Maendeleo na Ushirikiano wa Elimu ya Juu kati ya China na Afrika katika Zama za Kidijitali” limefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU.. Naibu Waziri wa Elimu wa China Bw. Wu Yan, Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Uvumbuzi wa Teknolojia ya Jamhuri ya Kongo Bi. Delphine Edith Emmanuel Adouki, Mkurugenzi wa Chin...
Tarehe 25 Julai, Baraza la Saba la Raia wa China na Afrika na Baraza la Viongozi Vijana wa China na Afrika yamefanyika katika mji wa Changsha, mkoa wa Hunan. Viongozi, wakuu, wawakilishi zaidi ya 200 kutoka nchi zaidi ya 50 wameshiriki kwenye mkutano. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CPC wa BFSU Prof. Jia Dezhong wamehudhuria ufunguzi.Umoja wa Hudu...