Mwanzo > Habari > Content

Li Hai Ateuliwa Katibu Mtendaji wa BFSU

Updated: 2025-11-19

Tarehe 19 Novemba, Chama cha CPC Shina la Wizara ya Elimu limeteua Bw. Li Hai kuwa Katibu Mtendaji wa CPC shina la BFSU na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo. Naibu Waziri wa Elimu Prof. Wang Jiayi amehudhuria kwenye mkutano na kutangaza uteuzi huo. Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu ya Wizara ya Elimu Bw. Ge Yuanjie, Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu la Beijing Bw. Yu Chengwen na Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian wamehudhuria mkutano huo.