HOME > Habari > Content

Naibu Waziri wa Elimu wa Kenya Atembelea BFSU

Updated: 2024-09-14

Tarehe 7 Septemba, Naibu Waziri wa Elimu wa Kenya Bi. Beatrice Muganda Inyangala na msafara wake wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua na Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian wamekutana na wageni na kuzungumzia mawasiliano ya utamaduni na ushirikiano wa elimu.

Prof. Wang Dinghua ameeleza matunda mapya ya BFSU katika usimamizi wa elimu ya dunia, maendeleo endelevu ya elimu na ujenzi wa chuo kikuu bora cha lugha za kigeni duniani. Bi. Inyangala amesifia michango ya BFSU katika kuendeleza utafiti na ufundishaji wa lugha, utamaduni na jamii za Afrika. Pia ametumai Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika utawajengea vijana majukwaa ukichangamkia fursa za zama ya kidijitali.

Baada ya mazungumzo, Bi. Inyangala na wageni wametembelea Makumbusho ya Lugha za Duniani ya BFSU.