Tarehe 27 Machi, Balozi wa Cambodia Nchini China Bi. Soeung Rathchavy ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amekutana na wageni. Wamezungumza kuhusu kutayarisha wanafunzi na wasomi wa ngazi ya juu na kukuza ushirikiano wa utafiti na utamaduni.

Kwa niaba ya Mama Malkia Monineath wa Cambodia, Balozi Rathchavy amezawadia BFSU vitabu. Jia Wenjian amepokea vitabu kwa niaba ya Chuo Kikuu. Wanafunzi wa kozi ya Kikhmer wameimba wimbo wa kumkaribisha balozi huyo.