Tarehe 28 Oktoba, Mshauri wa Chuo Kikuu cha Chicago Prof. John Boyer ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU na kutoa mhadhara wenye mada ya “Historia na Maendeleo ya ‘Elimu ya Kibinadamu’: Mfano wa Chuo Kikuu cha Chicago”. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua amekutana na mgeni huyo na msafara wake.
Tarehe 25 Oktoba, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Uruguay Prof. Julio Fernández Techera ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amekutana na mgeni huyo. Pande hizo mbili zimezungumia kuhusu utafiti wa Amerika ya Kilatini, uhusiano wa China na Amerika ya Kilatini, mawasiliano ya walimu na wanafunzi na masuala mengine.
Kuanzia tarehe 6 hadi 8 Oktoba, Kongamano la Viongozi wa Kimkakati wa Dunia la 2024 limefanyika mjini Guadalajara nchini Mexico. Kwa kufuata mwaliko wa Baraza la Shule za Shahada ya Uzamili na Uzamivu la Marekani, Mkuu wa Jumuiya ya Elimu ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu ya China Bw. Yang Wei ameongoza ujumbe kuhudhuria kongamano hilo. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian ameshiriki na kutoa ...
Tarehe 11 Oktoba, Spika wa Cyprus Bi. Annita Demetriou ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha BFSU na kutoa hotuba. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amemkaribisha. Baada ya kutoa hotuba, Bi. Demetriou amezungumza na kujibu maswali ya walimu na wanafunzi wa BFSU.
Kuanzia tarehe 22 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua ameongoza ujumbe kutembelea Marekani, Kuba na Panama. Amehudhuria kwenye Kongamalo la Wakuu wa Vyuo Vikuu “10+10” vya China na Marekani na kutoa hotuba. Wajumbe hawa pia wametembelea vyuo vikuu vya Marekani vikiwemo Chuo Kikuu cha Northwestern, Chuo Kikuu cha Chicago, Chuo Kikuu cha Stony ...
Tarehe 21 Septemba, sherehe ya kuzindua “Kiti cha Msomi wa Utafiti wa Malaysia cha Sultani Ibrahim” imefanyika. Mfalme wa Malaysia Ibrahim Sultan Iskandar ametia sahihi ya kuidhinisha. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Juu ya Malaysia Prof. Azlinda Azman, Balozi wa Malaysia nchini China Bw. Norman Muhamad, Waziri wa Usafiri wa Malaysia Bw. Loke Siew Fook na ...
Tarehe 20 Septemba, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Cologne, Mwenyekiti wa Kituo cha Mawasiliano ya Kiutafiti cha Ujerumani Bw. Joybrato Mukherjee ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua amekutana na mgeni huyo na msafara wake. Wamezungumzia utafiti, mawasiliano ya walimu na wanafunzi na masuala mengine.
Tarehe 15 Septemba, Chuo Kikuu cha BFSU kimeanzisha kozi ya Kitetum kwa mara ya kwanza nchini China. Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Zhao Gang, Mwambata wa Elimu wa Ubalozi wa Timor-Leste nchini China Bw. Rogério Paulo Chaves wamehudhuria ufunguzi wa darasa na kutoa hotuba kabla ya kipindi kuanza.
Tarehe 7 Septemba, Naibu Waziri wa Elimu wa Kenya Bi. Beatrice Muganda Inyangala na msafara wake wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua na Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian wamekutana na wageni na kuzungumzia mawasiliano ya utamaduni na ushirikiano wa elimu. Prof. Wang Dinghua ameeleza matunda mapya ya BFSU katika usimamizi wa elimu ya dunia, maende...