Tarehe 17 Machi, Mwalimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Keele Prof. Kevin Shakesheff na Makamu Mkuu Prof. Antonius Raghubansie wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian na Makamu Mkuu Prof. Zhao Gang wamekutana na wageni hawa. Wamezungumza kuhusu kuimarisha miradi ya elimu ya ushirika ikiwemo shahada ya kwanza ya masomo ya diplomasia na shahada ya uzamili ya teknolojia ya elimu na akili unde ili kupanua zaidi ushirikiano kati ya pande mbili.

Wajumbe wa Chuo Kikuu cha Keele wametembelea Kitivo cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa na Kitivo cha Elimu ya Mtandaoni ili kufanya mazungumzo na walimu na wanafunzi.