Mpaka Agosti 2024, baada ya kuchapishwa kwa kitabu cha “Elimu ya Juu ya China: Uchunguzi na Utafiti”, vitabu vyote sita vilivyoandikwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua vimechapishwa. Vitabu hivyo vilivyochapishwa na Shirika la Uchapishaji la Elimu ya Wananchi wa China ni pamoja na “Elimu ya Msingi ya China: Uchunguzi na Utafiti”, “Elimu ya Msingi ya Marekani: Uchunguzi na Utafiti”, “Elimu ya Juu ya China: Uchunguzi na Utafiti”, “Elimu ya Juu ya Marekani: Uchunguzi na Utafiti”, “Elimu ya Ualimu ya China: Uchunguzi na Utafiti” na “Elimu ya Ualimu ya Marekani: Uchunguzi na Utafiti”.