HOME > Habari > Content

Kongamano la Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika Lafanyika

Updated: 2024-09-14

Tarehe 5 Septemba, Kongamano la Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika lenye mada ya Maendeleo na Ushirikiano wa Elimu ya Juu kati ya China na Afrika katika Zama za Kidijitali limefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU.. Naibu Waziri wa Elimu wa China Bw. Wu Yan, Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Uvumbuzi wa Teknolojia ya Jamhuri ya Kongo Bi. Delphine Edith Emmanuel Adouki, Mkurugenzi wa China wa Umoja huo Bw. Zhou Yu na Wiziri wa Teknolojia na Elimu ya Juu wa Sierra Leone Bw. Ramatulai Wurie wamehudhuria na kutoa hotuba. Wawakilishi kutoka vyuo vikuu zaidi ya 80 vya China na Afrika wameshiriki kwenye kongamano.

Baada ya ufunguzi, hati za makubaliano 14 za elimu zimetiliwa saini na matunda ya ushirikiano yametolewa. Pia Jukwaa la Kidijitali la Ushirikiano wa Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika limeanzishwa. Wakurugenzi wa kiutendaji wa China na Afrika wa Umoja huo Prof. Wang Dinghua na Bw. Olusola Oyewole wametoa hotuba.

Mazungumzo matatu yenye mada maalum yamefanyika. Wadau mbalimbali wa elimu ya juu wamezungumza na kupeana maarifa kwa undani.