HOME > Habari > Content

Umoja wa Huduma ya Kujitolea Duniani Waanzishwa

Updated: 2024-08-27

Tarehe 25 Julai, Baraza la Saba la Raia wa China na Afrika na Baraza la Viongozi Vijana wa China na Afrika yamefanyika katika mji wa Changsha, mkoa wa Hunan. Viongozi, wakuu, wawakilishi zaidi ya 200 kutoka nchi zaidi ya 50 wameshiriki kwenye mkutano. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CPC wa BFSU Prof. Jia Dezhong wamehudhuria ufunguzi.

Umoja wa Huduma ya Kujitolea Duniani ulioanzishwa na BFSU pamoja na Mpango wa Elimu ya Kuwawezesha Wajasiriamali wanawake wa China na Afrika na Mradi wa Mafunzo ya AI kwa Vijana vimeorodheshwa katika Orodha ya matunda ya Mpango wa Urafiki wa Raia wa China na Afrika (2024-2026).