Tarehe 29 Juni hadi 9 Julai, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Dezhong ameongoza wajumbe kutembelea Ethiopia, Kenya na Tanzania. Wametembelea Chuo Kikuu cha Addis Ababa, Chuo Kikuu cha Nairobi, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na kufanya mazungumzo pamoja na wakuu wa vyuo husika.
Zaidi ya hayo, Prof. Jia Dezhong na wajumbe wametembelea makampuni ya China kama vile CCECC, CHEC, CGTN Africa, Startimes na baadhi ya mashirika ya kimataifa kama UN-Habitat na UNEP ili kuwatafutia wanafunzi nafasi za ajira na mafunzo kwa vitendo. Wajumbe hao pia wametembelea mabalozi ya China nchini Ethiopia na Kenya pamoja na ubalozi mdogo mjini Zanzibar.
Chama cha Wahitimu wa BFSU nchini Kenya na Kameroon vimeanzishwa vilevile.