Mwanzo > Habari > Content

Walimu wa Nchi za nje Kutoka BFSU Washiriki Tafrija ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani

Updated: 2026-03-06

Tarehe 6 Machi, tafrija ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani imefanyika mjini Beijing. Mjumbe wa Baraza la Serikali na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanawake la China Bi. Shen Yiqin ametoa hotuba. Baadhi ya wawakilishi wanawake wa Bunge la Umma la China na wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, wanawake mashuhuri wa makabila na nyanja mbalimbali, wanawake kutoka Hong Kong na Macao, baadhi ya mabalozi nchini China pamoja na wageni wa ndani na nje ya nchi wamehudhuria tafrija hiyo. Walimu wa kike 11 wa nchi za nje kutoka BFSU wamealikwa kuungana nao pia.