Mnamo tarehe 23 Mei, “Jukwaa la Maendeleo ya Tibet ya China la 2023” limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Beijing. Kaulimbiu ya jukwaa hilo ni "Zama Mpya, Tibet Mpya na Safari Mpya". Jukwaa hilo limeandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, Serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet pamoja na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing.Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang...
Mnamo tarehe 4 Mei, Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini China Bw. Ali Obaid Al Dhaheri ametembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na Bw. Dhaheri na msafara wake. Wamejadiliana juu ya kuimarisha ushirikiano katika kupelekeana wanafunzi, mafunzo ya pamoja na mawasiliano ya kitaaluma. Baada ya mkutano, Bw. Dhaheri ...
Kuanzia tarehe 16 hadi 23 Aprili, Makamu Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian ameongoza ujumbe kutembelea Jamhuri ya Czech na Jamhuri ya Italia. Wametembelea vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo Chuo Kikuu cha Palacký, Chuo Kikuu cha Roma cha Italia, Chuo Kikuu cha Mashariki cha Naples na kadhalika ili kuimarisha ushirikiano wa nyanja mbalimbali kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na vyuo vi...
Tarehe 9 Aprili, "Kamusi ya Sayansi ya Jamii ya Kichina-Kitibet-Kiingereza" imetolewa katika Taasisi ya Utafiti wa Tibet ya China mjini Beijing. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing pamoja na Shirika la Uchapishaji la Biashara.Kamusi ya Sayansi ya Jamii ya Kichina-Kitibet-Kiingereza ni matunda ya mradi mkubwa wa kimsingi wa utafiti wa sayansi ya jamii wa Tibet a...
Tarehe 3 Aprili, Mkurugenzi wa Ofisi ya Asia Mashariki ya Shirika la Msalaba Mwekundu Bw. Pierre Krähenbühl ametembelea BFSU. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amekutana na Bw. Pierre Krähenbühl na ujumbe wake.Pande hizo mbili zimejadiliana juu ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali zinazowahusisha wanafunzi zikiwemo kupata ajira, kutoa huduma ya kujitolea na mawasiliano ya kitaaluma....
Tarehe 31 Machi, Rais wa Chuo Kikuu cha Queensland cha Australia Bi. Deborah Terry ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amekutana na Bi. Deborah Terry na msafara wake. Pande hizo mbili zimetiliana saini "Mkataba wa Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na Chuo Kikuu cha Queensland".
Tarehe 23 Machi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Belarusi Bw. Andrei Karol ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amezungumza na Bw. Andrei Karol, na vyuo vikuu viwili vimetilia saini mkataba wa kupelekeana wanafunzi.
Tarehe 20 Machi, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kifaransa yamefanyika kwenye Ubalozi wa Ufaransa nchini China. Wizara ya Elimu ya Ufaransa imemtunukia Mkuu wa Kitivo cha Kifaransa cha BFSU Prof. Dai Dongmei tuzo ya Academic Palm Knight kwa kuzingatia mchango wake katika kuendeleza elimu ya Kifaransa na kueneza utamaduni wa Kifaransa. Balozi mpya wa Ufaransa nchini China Bw. Bertra...
Tarehe 20 Machi, Balozi wa Kazakhstan nchini China Bw. Shakhrat Nuryshev ametembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya kwanza ya kitaifa ya lugha ya Kikazakh. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na Bw. Shakhrat Nuryshev na msafara wake. Wamefanya mazungumzo ya kina kuhusu ushirikiano wa kutoa mafunzo ya tafsiri na ukal...