Mwanzo > Habari > Content

Balozi wa Uruguay Atembelea BFSU

Updated: 2025-12-24

Tarehe 24 Desemba, Balozi wa Uruguay nchini China Bw. Aníbal Cabral ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Zhao Gang wamekutana na wageni.

Prof. Jia ameeleza habari za maendeleo ya taaluma, mawasiliano ya kimataifa na ujenzi wa kozi ya Kihispania wa BFSU. Amesema Chuo Kikuu cha BFSU kinazingatia sana mawasiliano na nchi za Amerika ya Kilatini ikiwemo Uruguay, na kinatumai kuimarisha uelewano na urafiki baina ya nchi mbili kwa kupitia ushirikiano wa elimu na mazungumzo kati ya vijana.

Bw. Cabral amesifia BFSU kwa maendeleo yake katika kutayarisha wanafunzi na wasomi wenye maono ya kimataifa na kuzidisha mawasiliano ya watu baina ya nchi mbili. Pia ametarajia kuzidisha mawasiliano ya vijana na kuimarisha ushirikiano wa utafiti, elimu na utamaduni katika siku za mbele.