Mwanzo > Habari > Content

Kamusi ya Sayansi ya Jamii ya Kichina-Kitibet-Kiingereza yatolewa

Updated: 2023-05-03

Tarehe 9 Aprili, "Kamusi ya Sayansi ya Jamii ya Kichina-Kitibet-Kiingereza" imetolewa katika Taasisi ya Utafiti wa Tibet ya China mjini Beijing. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing pamoja na Shirika la Uchapishaji la Biashara.

Kamusi ya Sayansi ya Jamii ya Kichina-Kitibet-Kiingereza ni matunda ya mradi mkubwa wa kimsingi wa utafiti wa sayansi ya jamii wa Tibet ambayo imehaririwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan pamoja na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Tibet, BFSU na Chuo Kikuu cha Fedha na Uchumi cha Kusini Magharibi. Hiyo ni kamusi ya kwanza ya sayansi ya jamii inayohaririwa kwa lugha tatu za Kichina, Kitibeti na Kiingereza, na misamiati mingi ya isimu, sanaa na akiolojia imepangwa kwa utaratibu na kutafsiriwa katika Kitibet kwa mara ya kwanza. Kamusi ina juzuu 21 na maneno zaidi ya 45,000.