Mwanzo > Habari > Content

Balozi wa Kazakhstan nchini China atembelea BFSU

Updated: 2023-04-07

Tarehe 20 Machi, Balozi wa Kazakhstan nchini China Bw. Shakhrat Nuryshev ametembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya kwanza ya kitaifa ya lugha ya Kikazakh. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na Bw. Shakhrat Nuryshev na msafara wake. Wamefanya mazungumzo ya kina kuhusu ushirikiano wa kutoa mafunzo ya tafsiri na ukalimani, kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wageni na kadhalika.