Tarehe 20 Machi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Western Sydney cha Australia Bw. Barney Glover ametembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na Bw. Barney Glover na msafara wake. Wamejadiliana juu ya mawasiliano ya wanafunzi na walimu wa pande mbili, mafunzo ya pamoja, programu za shahada ya uzamili na kadhalika.