Mwanzo > Habari > Content

Mkurugenzi wa Ofisi ya Asia Mashariki ya Shirika la Msalaba Mwekundu Atembelea BFSU

Updated: 2023-05-03

Tarehe 3 Aprili, Mkurugenzi wa Ofisi ya Asia Mashariki ya Shirika la Msalaba Mwekundu Bw. Pierre Krähenbühl ametembelea BFSU. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amekutana na Bw. Pierre Krähenbühl na ujumbe wake.

Pande hizo mbili zimejadiliana juu ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali zinazowahusisha wanafunzi zikiwemo kupata ajira, kutoa huduma ya kujitolea na mawasiliano ya kitaaluma. Bw. Pierre Krähenbühl ametoa mhadhara maalum unaohusu misaada ya kibinadamu kwa walimu na wanafunzi wa BFSU.