Mwanzo > Habari > Content

Rais wa Uruguay Atembelea BFSU

Updated: 2026-02-04

Tarehe 4 Februari, Rais wa Uruguay Mhe. Yamandu Orsi ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Bw. Li Hai, Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Zhao Gang, pamoja na Balozi wa China nchini Uruguay Bw. Huang Yazhong, Mwambata wa Idara ya Amerika ya Kilatini na Caribbean ya Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Zhang Wenwei, Naibu Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Mawasiliano ya Kimataifa ya Wizara ya Elimu Bw. Zhang Jin wamekutana na wageni.

Saa 3:00 asubuhi, Rais Orsi, Li Hai na Jia Wenjian wameweka udongo mpya na kumwagilia maji mti wa urafiki kati ya China na Uruguay uliopandwa mwaka 2013 na Rais wa zamani wa Uruguay, Mhe. Mujica. Pia wamezindua bango jipya la mti wa urafiki.



Rais Orsi wamezungumza na walimu na wanafunzi kutoka vyuo vikuu na shule za sekondari 16 zinazofundisha lugha ya Kihispania mjini Beijing. Bw. Li Hai amewakaribisha wageni kwa niaba ya Chuo Kikuu cha BFSU. Alisema kuwa BFSU imekuwa na ushirikiano wa karibu na Uruguay kwa muda mrefu, na inatarajia kuimarisha zaidi ushirikiano na vyuo vikuu na taasisi za kitaaluma nchini Uruguay, ili kutayarisha vijana wengi zaidi wanaoelewa lugha na tamaduni za pande mbili.

Katika hotuba yake, Rais Orsi ameeleza kuwa msingi wa uhusiano kati ya nchi mbili ni kuaminiana. Katika muktadha huu, mawasiliano ya kitaaluma yanabeba jukumu muhimu. Anatumaini kwamba pande mbili zinaweza kufundishana, kuvuka mipaka ya ujuzi, na kukuza amani na maendeleo kupitia ushirikiano na mazungumzo.

Li Hai amemzawadia Rais Orsi mchoro wa mti wa urafiki kati ya China na Uruguay uliochorwa na wanafunzi wa Kitivo cha Kihispania na Kireno cha BFSU.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uruguay Bw. Lubetkin, Balozi wa Uruguay nchini China Bw. Cabral, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Fratti, Waziri wa Viwanda, Nishati na Madini Bw. Cardona wamehudhuria shughuli hiyo.