Mwanzo > Habari > Content

BFSU yatembelea Czech na Italia

Updated: 2023-05-10

Kuanzia tarehe 16 hadi 23 Aprili, Makamu Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian ameongoza ujumbe kutembelea Jamhuri ya Czech na Jamhuri ya Italia. Wametembelea vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo Chuo Kikuu cha Palacký, Chuo Kikuu cha Roma cha Italia, Chuo Kikuu cha Mashariki cha Naples na kadhalika ili kuimarisha ushirikiano wa nyanja mbalimbali kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na vyuo vikuu hivyo. Wametembelea ubalozi wa China nchini Czech na ubalozi wa China nchini Italia na kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa ubalozi. Pia wametembelea baadhi ya wahitimu na wanafunzi wa BFSU nchini Italia.