Mwanzo > Habari > Content

Li Hai Ahudhuria Kongamano la Pili la Maendeleo ya Elimu baina ya China na Ufaransa

Updated: 2025-12-05

Tarehe 5 Desemba, Wizara ya Elimu ya China na Wizara ya Elimu ya Juu, Utafiti na Shughuli za Anga ya Juu ya Ufaransa zimeandaa kwa pamoja Kongamano la Pili la Maendeleo ya Elimu baina ya China na Ufaransa mjini Chengdu, mkoani Sichuan. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Bw. Li Hai amehudhuria kongamano hilo na kutoa hotuba yenye mada ya “Kujenga Mfumo wa Kutayarisha Wasomi wa Siku za Mbele ili Kusukuma Mbele Maendeleo Endelevu”.