Mwanzo > Habari > Content

Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini Atembelea BFSU

Updated: 2025-12-03

Tarehe 3 Desemba, Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini Bw. Gayton Mckenzie na msafara wake wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Liu Xinlu wamekutana na wageni hao. Wamezungumzia mawasiliano ya walimu na wanafunzi, utafiti wa pamoja, tafsiri za kazi za fasihi, ushirikiano wa sanaa na pande mbalimbali.