Tarehe 21 Novemba, Kongamano la Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Asia (AUPF) limefanyika jijini Guangzhou. Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni “Teknolojia Mpya na Ushirikiano wa Sekta Mtambuko: Kutafuta Njia Mpya ya Maendeleo Jumuishi ya Elimu ya Juu barani Asia”. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amehudhuria Kongamano hilo na kutoa hotuba yenye mada ya “Daraja la Mawasiliano Duniani: Jukwaa la Huduma ya Lugha la Dunia la Chuo Kikuu cha BFSU”.