CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Idara ya Kihispania na Kireno

发布时间:2019-04-28

Tangu kuanzishwa kwa taaluma ya Kihispania mwaka 1952 na taaluma ya Kireno mwaka 1961,  BFSU imekuwa ikiongoza katika miaka yote 60 iliyopita kwa vile programu za M.A (1979) na Ph.D (1996) zote zilianzishwa kwa mara ya kwanza nchini China.

Hadi sasa idara hiyo ina walimu wa Kihispania 25 wakiwemo maprofesa 4, maprofesa washiriki 5 na wataalamu wawili kila mwaka. Na ina walimu wa Kireno wanane wakiwemo wataalamu wawili.

Kwa taaluma ya Kihispania programu ya M.A ni ya miaka mitatu katika fani za Isimu, Fasihi, Tafsiri na Ukalimani na Uchunguzi wa Nchi za Kihispania. Programu ya Ph.D ni kati ya miaka 3-4 katika Fasihi ya Latin-Amerika na Ukalimani. Taaluma ya Kireno ina programu ya M.A tu ambayo ni ya miaka mitatu katika fani mbili: Tafsiri na Ukalimani; Sera ya Mambo ya Nje ya Brazil na Uhusiano wa China na Brazil.

Katika miaka 60 iliyopita, idara hii imetayarisha wanafunzi 3,000 wenye umahiri wa lugha, ujuzi mpana na maadili mema ambao wametoa mchango mkubwa katika kukuza urafiki na ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kati ya China na nchi za Kihispania na Kireno. Wengi wao wamekuwa wanadiplomasia, wakalimani, maprofesa, waandishi wa habari n.k.

Idara hii inatilia mkazo ushirikiano na vyuo vikuu vya nchi za Kihispania na Kireno na kila mwaka inawapeleka walimu na wanafunzi kusomea ng’amboni. Idara hii imejenga “Kituo cha Utafiti wa Mexico” ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Kujiendesha cha Mexico na “Shirikisho la Mawasiliano ya Lugha na Utamaduni kati ya China na Nchi za Kireno” ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Lisbon.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC