CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Maktaba

MAKTABA

2019年04月16日


1 (3)

Maktaba ya BFSU ni jengo la alama lenye ghorofa 6 na eneo lake linafikia mita za mraba 23,000. Ukuta wake wa nje umepambwa na neno “MAKTABA” kwa lugha 55 tofauti nao unaonesha upekee na upeo mpana wa utamaduni wa chuo. Paa la kioo juu ya jengo hilo linapelekea humu ndani kuonekana kama “bahari ya ujuzi” endapo miale ya jua ikipiga. Ngazi iliyomo katikati mithili ya “mlima wa vitabu” inabainisha usemi wa Kichina – “Bidii ndio njia pekee inayokufikisha kikomo cha hekima”. Pamoja na mpangilio rahisi na eneo lililo wazi kabisa, maktaba nzima inadhihirisha uwazi na usasa wake ambao unaleta maelewano baina ya watu na vitabu.

_MG_6879 副本

Maktaba inahifadhi vitabu vipatavyo 1,264,000 na vitabu pepe 482,000, majarida 1,174 ya Kichina na ya lugha za kigeni na database 56 hasa katika vipengele vya lugha, fasihi na utamaduni. Sambamba na ukuaji wa mitalaa mtambuko, machapisho ya sheria, diplomasia, uchumi, uandishi wa habari na usimamizi yamekusanywa kibao miaka ya karibuni.

_MG_6921 副本

Mbali na sehemu za kukaa zaidi ya 2,000 na vyumba 8 vya kusomea, maktaba ina vyumba vya mikutano, vyumba vya mihadhara, ukumbi wa maonesho na mgahawa, vyote ambavyo vimeipelekea maktaba hii siyo mahala pa kujipatia elimu tu, bali ni kuwasiliana na kusikilizana baina ya watu. Maktaba imeweka mashine ya kurudishia vitabu masaa 24 pamoja na huduma nyingine kama kuchapa, kunakili, kuskani n.k. Matumizi ya vifaa vya multimedia na teknolojia ya kimambo leo yanasaidia sana kuboresha usimamizi na huduma yetu, kadhalika kwenda sambamba na maendeleo kasi katika zama za maarifa tunazoishi.

1DX_2813

Yote hayo ya hazina kubwa, mazingira murua, huduma bora na vifaa vya kisasa yameipelekea maktaba yetu iwe mahala pa kuvutia walimu na wanafunzi kusoma, kutafiti na kuwasiliana baina yao humu ndani.No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC