CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

KUHUSU BFSU

2019年04月15日


Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing kipo kwenye sehemu ya kaskazini ya Barabara ya Xisanhuan ambayo inatenganisha chuo katika kampasi ya mashariki na ya magharibi. Chuo chetu kinaongozwa na Wizara ya Elimu moja kwa moja na ni kimojawapo cha vyuo vikuu vilivyopewa kipaumbele katika miradi ya “211” na “985” ya kitaifa. Chuo chetu kinaongoza ufundishaji wa lugha za kigeni nchini China kwa historia yake ndefu, wingi wa lugha za kufundishia na ukamilifu wa mitalaa.

Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing kiliasisiwa mwaka 1941 ambapo kilikuwa idara ya Kirusi ya chuo kikuu cha kijeshi mjini Yan’an. Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, chuo chetu kikawa chini ya uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje hadi mwaka 1980. Mnamo mwaka 1994, chuo kilipandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Hivi sasa chuo kikuu kinafundisha aina 98 za lugha za kigeni na kinaweza kutunukia shahada za uzamivu za Lugha na Fasihi za Kigeni, Lugha na Fasihi ya Kichina, Uandishi na Mawasiliano ya Habari, Sayansi ya Siasa, Sheria, Sayansi ya Menejimenti na nyinginezo.

Chuo chetu kilikuwa kinakwenda sambamba na maendeleo ya taifa katika miaka 76 iliyopita na kimekuwa kitovu muhimu ambacho kimeandaa wahitimu bora wapatao elfu 90 ambao wanafanya kazi katika sekta za diplomasia, tafsiri, uchumi, biashara, vyombo vya habari, sheria, fedha n.k. Kwa mfano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, inakadiriwa kuwa wapatao mabalozi 400 na mabalozi wadogo 1,000 na ushei walihitimu kutoka chuo chetu kiasi kwamba chuo kimesifika kama ni “Mlezi wa Wanadiplomasia wa Jamhuri”.
No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC