CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Idara ya Kijapani

Idara ya Kijapani ilizinduliwa mwaka 1956 na ilianzisha programu ya M.A mwaka 1986 na programu ya Ph.D mwaka 1993. Tangu mwaka 2008 idara hii imeorodheshwa kama mmojawapo wa mitalaa ya kitaifa na Wizara ya Elimu.

Katika idara hii kuna walimu 22 wakiwemo maprofesa 3, maprofesa washiriki 12 na wahadhiri 7. Kati yao walimu 17 ni wazamivu na wengine 4 ni wazamili. Isitoshe, idara hii inawaalika wataalamu wawili wa lugha na maprofesa wawili kutoka Japani.

Kila mwaka idara hii inasajili wanafunzi 74 wa shahada ya kwanza ambao 2/3 ya hao hawana msingi wowote huku 1/3 wamejifunza Kijapani kwenye shule za sekondari. Aidha, inadahili wanafunzi 20 wa M.A na 3-4 katika programu ya Ph.D.

Mbali na mafunzo thabiti ya lugha, wanafunzi wanapata kunolewa mambo mbali mbali ya Japani kupitia kozi na semina katika mwaka wa tatu na wa nne. Wanafunzi mahiri wanahamasishwa kujiunga na programu nyingine za biashara, diplomasia, sheria n.k. katika BFSU.

Kwa upande wa ushirikiano wa kimataifa, idara hii imeingia mkataba wa ushikiano na Chuo Kikuu cha Waseda, Chuo Kikuu cha Kobe, Chuo Kikuu cha Okayama, Chuo Kikuu cha Gakushuin, Chuo Kikuu cha Rikkyo,  Chuo Kikuu cha Aoyama, Chuo Kikuu cha Kansai, Chuo Kikuu cha Bunkyo, Chuo Kikuu cha Daito Bunka, Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Nagoya, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Nagasaki Junshin na Chuo Kikuu cha Kobe Shoin. Kila mwaka wanafunzi 26-28 wanapelekwa vyuo hivi kusoma.

Kituo cha Utafiti wa Japani cha Beijing

Kituo cha Utafiti wa Japani cha Beijing kinachosimamiwa na Wizara ya Elimu na Mfuko wa Japani kiliasisiwa mwaka 1985. Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, kituo hiki kimewaandaa wasomi mahiri zaidi ya 1, 000 katika fani ya utafiti wa Japani.

Kama ni mtalaa wa kitaifa na kituo cha utafiti wa kikanda, kituo hiki kina programu za M.A na Ph.D zenye vipengele sita ambavyo ni: Isimu ya Kijapani, Ufundishaji wa Kijapani, Fasihi ya Kijapani, Utamaduni wa Japani, Jamii ya Japani na Uchumi wa Japani. Hivi sasa wapo wanafunzi 109 wa M.A, wanafunzi 47 wa Ph.D na wasomi na watafiti kadha wa kadha kutoka ndani na nje ya nchi.

Kituo hiki kinashirikiana kwa karibu na wasomi mashuhuri wa Japani wanaotumwa na Mfuko wa Japani kila mwaka pamoja na wasomi wazalendo wanaoalikwa.

Mbali na wasomi, kituo hiki kinashirikiana na Chuo Kikuu cha Kobe na Chuo Kikuu cha Okayama katika kuwafunza wanafunzi wa shahada ya uzamili. Hali kadhalika, kituo hiki kimeingia mkataba wa ushirikiano na vyuo vikuu na taasisi 23 za Japani ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu vya Tokyo, Ochanomizu, Waseda, Mie, Nagoya, Shinshu na Taasisi ya Kijapani ya Taifa na ya Fasihi ya Kijapani ya Taifa.

Maktaba ya kituo hiki inahifadhi vitabu vipatavyo elfu 170 kiasi kwamba imezidi maktaba zote za aina hii nchini humo.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC