Mwanzo > Habari > Content

Malkia wa Uhispania Atembelea BFSU

Updated: 2025-11-14

Tarehe 13 Novemba, Malkia wa Uhispania Letizia Ortiz Rocasolano ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Naibu Waziri wa Elimu Bw. Ren Youqun, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Mawasiliano ya Kimataifa Bw. Yang Dan, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Zhao Gang wamekutana na wageni hao.

Malkia Letizia na viongozi wengine wamezindua bango la kumbukumbu linalotoa heshima na shukurani kwa walimu wa Uhispania waliokuja kufundisha Kihispania katika miaka ya 1950.

Mkuu wa Kitivo cha Kihispania na Kireno Prof. Chang Fuliang ameeleza historia na maendeleo ya taaluma ya Kihispania ya BFSU na vyuo vingine nchini. Na Malkia Letizia amezungumza na walimu na wanafunzi wa BFSU katika hali ya kirafiki.