Mwanzo > Habari > Content

Mazungumzo ya Vyuo Vikuu kuhusu Utekelezaji wa “Makubaliano ya Mustakabali” Yafanyika BFSU

Updated: 2025-10-31

Tarehe 16 Oktoba, Mazungumzo ya Vyuo Vikuu kuhusu Utekelezaji wa Makubaliano ya Mustakabali yamefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU. Naibu Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Wizara ya Elimu Bw. Li Hai, Naibu Katibu Mkuu wa Sera wa Umoja wa Mataifa Bw. Guy Ryder, Mkuu wa Idara ya Utekelezaji wa Makubaliano ya Mustakabali wa Umoja wa Mataifa Bw. Themba Kaula, Afisa Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa Bw. Siddharth Chatterjee, mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua wamehudhuria kwenye ufunguzi na kutoa hotuba.

Mada ya mazungumzo hayo ni Kutekeleza Makubaliano ya Mustakabali, Kuboresha Utawala wa Dunia. Wawakilishi kutoka Vyuo Vikuu duniani, Wizara ya Elimu na Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Shirikisho la Taifa la Vijana wa China, maafisa wa Umoja wa Mataifa wameshiriki mazungumzo hayo na kuzindua rasmi Mpango wa Utekelezaji wa Makubaliano ya Mustakabali wa Vyuo Vikuu.