Mwanzo > Habari > Content

Kongamano la Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Lugha za Kigeni Duniani Lafanyika Hangzhou

Updated: 2025-10-31

Tarehe 24 Oktoba, Kongamano la Tano la Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Lugha za Kigeni Duniani (GAFSU) limefanyika katika Hangzhou. Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Elimu ya China Bw. Liu Limin, mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian, mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Zhejiang Prof. Zhang Huanzhou na wakuu wengine wamehudhuria kwenye kongamano hilo.

Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni Mustakabali wa Maendeleo kwa Kutegemea Dijitali. Wataalamu na wanachuoni zaidi ya 170 kutoka nchi 27 wameshiriki kwenye kongamano hilo ambalo limepitisha Pendekezo la Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Elimu na Utafiti wa Lugha katika Zama ya Kidijitali.