Mwanzo > Habari > Content

Makamu wa Rais wa Bulgaria Atembelea BFSU

Updated: 2025-10-16

Tarehe 15 Oktoba, Makamu wa Rais wa Bulgaria Bi. Iliana Iotova ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amekutana na mgeni huyo na msafara wake. Prof. Jia Wenjian ameeleza habari fupi za BFSU na matumaini ya BFSU ya kushirikiana na serikali ya Bulgaria na ubalozi wake nchini China. Bi. Iotova amesisitiza umuhimu wa taaluma ya kibinadamu na kutoa matumaini ya serikali ya Bulgaria ya kushirikiana na BFSU kwa pamoja ili kudumisha urafiki wa Bulgaria na China.

Baada ya mazungumzo, Bi. Iotova ametoa hotuba kwa walimu na wanafunzi wa BFSU na kuzungumza nao. Pia amemtunukia Bw. Ma Xipu medali ya Saints Cyril and Methodius ya Bulgaria ili kumsifia mchango wake katika kueneza historia na utamaduni wa Bulgaria nchini China.