Tarehe 1 Septemba, sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa 2025 imefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU. Wanafunzi 3,917 kutoka nchi na kanda 90 wamejiunga na chuo hiki.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian, manaibu makatibu wakuu Prof. Jia Dezhong na Prof. Su Dapeng, makamu wakuu Prof. Ding Hao na Prof. Zhao Gang, Balozi wa Georgia nchini China Bw. Paata Kalandadze, mhitimu wa mwaka 2017 wa Kitivo cha Biashara ya Kimataifa Bw. Wang Yuhao wamehudhuria kwenye sherehe hiyo.
Prof. Jia Wenjian amewakaribisha wanafunzi wapya katika hotuba. Bw. Paata Kalandadze, wawakilishi wa wahitimu, walimu na wanafunzi wametoa hotuba.
