Mwanzo > Habari > Content

Mkuu wa SOAS Atembelea BFSU

Updated: 2025-09-02

Tarehe 29 Agosti, Mkuu wa SOAS Prof. Adam Habib na msafara wake wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua na Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian wamekutana na wageni hawa. Pande hizo mbili zimetia saini mkataba wa ushirikiano wa kujenga skuli ya pamoja.

Wageni hawa wametembelea makumbusho ya historia ya BFSU na shughuli za kuwapokea wanafunzi wapya wa mwaka 2025. Pia Prof. Adam Habib ametoa hotuba yenye mada ya Sisi Tuko Wapi? Afrika Kusini na Afrika katika Dunia ya Sasa.