Tarehe 21 hadi 29 Agosti, mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua ameongoza ujumbe kutembelea Iceland, Denmark na Uswidi. Wajumbe hawa wametembelea Chuo Kikuu cha Iceland na Taasisi yake ya Confucius, Chuo Kikuu cha Akureyri, Chuo Kikuu cha Aarhus, Chuo Kikuu cha Copenhagen, Chuo Kikuu cha Lund na Jumuiya ya Elimu ya Mawasiliano ya Nje ya Uswidi (Svenska Institutet).
Wajumbe hao pia wametembelea mabalozi ya China katika nchi hizo, Benki ya China Tawi la Stockholm na kituo cha utafiti cha Ulaya cha Kampuni ya Umeme wa Upepo ya Shanghai. Vilevile wametembelea wanafunzi wa BFSU wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Iceland na wahitimu wanaofanya kazi katika Denmark na Uswidi.
