Mwanzo > Habari > Content

Kambi ya Majira ya Joto ya Daraja la Kichina ya 2025 Yafunguliwa BFSU

Updated: 2025-08-13

Tarehe 31 Julai, kambi ya majira ya joto ya Daraja la Kichina ya 2025 imefunguliwa katika Chuo Kikuu cha BFSU. Naibu Katibu Mkuu wa CPC wa BFSU Prof. Jia Dezhong, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Ushirikiano na Mawasiliano ya Lugha cha China na Nchi za Nje Bw. Liu Jianqing wamehudhuria na kutoa hotuba kwenye hafla ya ufunguzi. Walimu na wanafunzi 154 kutoka nchi 15 wameshiriki katika kambi hiyo.

Kambi ya majira ya joto ya Daraja la Kichina inaandaliwa na BFSU pamoja na Kituo cha Ushirikiano na Mawasiliano ya Lugha cha China na Nchi za Nje. Kambi hiyo inalenga kuimarisha maelewano ya kimataifa na mawasiliano ya tamaduni na kutoa mafunzo bora ya Kichina kwa wanafunzi wa vyuo vikuu duniani.