Mwanzo > Habari > Content

Prof. Jia Wenjian Atembelea Rwanda, Uganda na Kenya

Updated: 2025-07-10

Tarehe 22 Juni hadi tarehe 1 Julai, mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian ameongoza ujumbe kutembelea Rwanda, Uganda na Kenya. Wajumbe hawa wametembelea Chuo Kikuu cha Rwanda, Chuo Kikuu cha Makerere, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Luyanzi, Kituo cha Uchunguzi wa Maendeleo cha Uganda, Chuo Kikuu cha Kenyatta na Chuo Kikuu cha Nairobi.

Wajumbe hawa pia wametembelea balozi za China katika nchi hizo tatu, CCECC Rwanda, kikosi cha madaktari wa China nchini Rwanda, Startimes Uganda, CCECC Kenya, Shirika la Habari la Xinhua katika Kenya na CRBC Kenya. Tena wameshiriki na kufungua makongamano yaliyoandaliwa na BFSU pamoja na Kituo cha Uchunguzi wa Maendeleo cha Uganda na Chuo Kikuu cha Nairobi.

Hii ni mara ya kwanza kwa BFSU kufanya ziara rasmi katika Rwanda na Uganda. Ujumbe wa BFSU umezungumzia kuimarisha ufundishaji wa lugha na tamaduni za Afrika na kutayarisha wanafunzi, kufanya utafiti pamoja na wataalamu wa nchi hizo tatu, kushirikiana na makampuni ya China na kuwatafutia wanafunzi nafasi za mafunzo kwa vitendo. Pia wametia saini makubaliano ya ushirikiano na pande husika.