Mwanzo > Habari > Content

Naibu Waziri wa Elimu wa Malaysia Atembelea BFSU

Updated: 2025-06-26

Tarehe 18 Juni, Naibu Waziri wa Elimu wa Malaysia Bw. Wong Kah Woh ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa Chuo Prof. Jia Wenjian na makamu mkuu Prof. Zhao Gang wamekutana na wageni hawa.

Prof. Jia Wenjian ameeleza habari fupi za BFSU na matumaini ya BFSU ya kushirikiana na pande mbalimbali za Malaysia. Bw. Wong Kah Woh amesema kwamba, Wizara ya Elimu ya Malaysia inatilia maanani mawasiliano na BFSU, na inatumai kushirikiana na BFSU katika mitihani ya lugha, mawasiliano ya walimu na wanafunzi na utafiti wa pamoja.

Baada ya mazungumzo, wajumbe hao wametembelea ofisi ya Kimalay na kituo cha utafiti.