Mwanzo > Habari > Content

Spika wa Bunge la Thailand Atembelea BFSU

Updated: 2025-06-26

Tarehe 23 Juni, spika wa bunge la Thailand Bw. Wan Muhamad Noor Matha ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU Prof. Wang Dinghua na makamu mkuu Prof. Zhao Gang wamekutana na wageni hawa.

Prof. Wang Dinghua amesema kwamba, tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita, uhusiano wa China na Thailand umeendelea kuwa imara. Mawasiliano haya yamechangia kuzidisha maelewano na kudumisha urafiki wa pande mbili. Bw. Wan Muhamad Noor Matha amesifu mchango wa BFSU katika kudumisha urafiki wa China na Thailand. Ameahidi kuendelea kuunga mkono mawasiliano ya vijana.

Baadaye Bw. Wan Muhamad Noor Matha amezungumza na walimu na wanafunzi wa BFSU.