Mwanzo > Habari > Content

Prof. Jia Wenjian Atembelea Brazil

Updated: 2025-06-09

Tarehe 2 hadi 6 Juni, mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian ameongoza ujumbe kutembelea Brazil. Wajumbe hawa wamehudhuria Mazungumzo ya Wakuu wa Vyuo Vikuu vya China na Brazil na kutembelea ubalozi wa China nchini Brazil. Pia wametembelea Chuo Kikuu cha Umoja wa Amerika Kusini na serikali ya mji wa Foz do Iguaçu.

Katika mazungumzo hayo, Prof. Jia Wenjian ametia saini makubaliano pamoja na Chuo Kikuu cha Umoja wa Amerika ya Kilatini na kutoa hotuba yenye mada ya Mazungumzo ya Dunia na Mawasiliano ya Tamaduni: Maarifa ya BFSU.