Mwanzo > Habari > Content

Prof. Jia Wenjian Ahudhuria Mikutano

Updated: 2025-05-21

Tarehe 11 hadi 13 Mei, Mkutano wa Nane wa Ushirikiano wa Elimu wa China na Belarusi, Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Elimu wa China na nchi za Asia ya Kati, kikao cha mwaka 2025 cha vyuo vikuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai(SCO), Baraza la Tisa la Mawaziri wa Elimu la SCO vimefanyika Urumqi, Xinjiang. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian amehudhuria mikutano hiyo.

Tarehe 11, Mkutano wa Nane wa Ushirikiano wa Elimu wa China na Belarusi umefanyika. Naibu Waziri wa Elimu wa China Bw. Wu Yan na Waziri wa Elimu wa Belarusi Bw. Andrei Ivanets wamehudhuria mkutano huo na Kituo cha Ushirikiano wa Utamaduni wa China na Belarusi kimeanzishwa kwenye mkutano huo.

Tarehe 12, Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Elimu wa China na nchi za Asia ya Kati limefanyika. Waziri wa Elimu wa China Bw. Huai Jinpeng ametoa hotuba. Prof. Jia Wenjian na Waziri wa Elimu na Sayansi wa Kyrgyzstan Bw. Dogdurkul Kendirbaeva wametia saini Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha BFSU na Wizara ya Elimu na Sayansi ya Kyrgyzstan.

Tarehe 12 hadi 13, kikao cha mwaka 2025 cha SCO kimefanyika. Prof. Jia Wenjian amehudhuria ufunguzi, na mkuu wa Kitivo cha Kirusi cha BFSU Prof. Dai Guiju ametoa hotuba kwenye kongamano la elimu ya kidijitali.

Tarehe 13, Baraza la Mawaziri wa Elimu la SCO limefanyika. Katika Baraza hilo, Umoja wa Elimu ya Kidijitali wa Nchi za SCO na Kituo cha Ubunifu wa Utayarishaji wa Wanafunzi wa Shahada ya Uzamifu wa China-SCO vimeanzishwa pia.