Mwanzo > Habari > Content

Prof. Jia Wenjian Atembelea Nchi Tatu za Asia ya Kati

Updated: 2025-05-06

Tarehe 16 hadi 24 Aprili, mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian ameongoza ujumbe kutembelea Kazakhstan, Uzbekistan na Kyrgyzstan. Wajumbe hawa wametembelea Chuo Kikuu cha Taifa cha Al-Farabi Kazakh, Chuo Kikuu cha Mahusiano ya Kimataifa na Lugha za Dunia cha Kazakh Ablai Khan, Chuo Kikuu cha Nazarbayev, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Utalii na Masalio ya Kitamaduni ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, Chuo Kikuu cha Taifa cha Lugha na Fasihi cha Alisher Navoi, Chuo Kikuu cha Taifa cha Mirzo Ulugbek; Chuo Kikuu cha Jusup Balasagyn Kyrgyz na Chuo Kikuu cha Taifa cha Bishkek.

Licha ya hayo, wajumbe hao wametembelea mabalozi ya China katika nchi tatu na ubalozi mdogo wa China mjini Alma-Ata. Pia wametembelea Wizara ya Elimu na Sayansi ya Kyrgyzstan, Kampuni ya Maendeleo ya Viwanda ya Pengsheng na Kampuni ya Reli ya Kyrgyzstan.

Hii ni mara ya kwanza kwa BFSU kufanya ziara katika Uzbekistan na Kyrgyzstan. Pande zote zimezungumzia kuimarisha ufundishaji na kutayarisha wanafunzi wa lugha rasmi za nchi tano za Asia ya Kati, kushirikiana katika utafiti wa kanda na nchi pamoja na vyuo vikuu maarufu vya Asia ya Kati, kutayarisha wafasiri wa Kirusi, Kichina na lugha za Asia ya Kati kwa pamoja, na kuhamasisha walimu na wanafunzi wa Asia ya Kati kujifunza nchini China. Pia wametia saini makubaliano ya ushirikiano.