Tarehe 16 Aprili, balozi wa Uswidi nchini China Bw. per Augustsson ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na wageni hawa. Wamezungumzia kuimarisha ushirikiano kati ya BFSU na pande za Uswidi, kuendeleza mawasiliano ya walimu na wanafunzi na kukuza utafiti.
Kabla ya kukutana na viongozi wa BFSU, Bw. Augustsson amefanya mazungumzo na walimu na wanafunzi wa kozi ya Kiswidi.
