Mwanzo > Habari > Content

Wang Dinghua Atembelea Austria, Uswisi na Ureno

Updated: 2025-04-02

Tarehe 20 hadi 29 Machi, mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua ameongoza ujumbe kutembelea Austria, Uswisi na Ureno. Wajumbe hawa wametembelea Kituo cha Utafiti cha Jellinek cha Austria, Chuo Kikuu cha Vienna na taasisi yake ya Confucius, Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo ya Geneva, Chuo Kikuu cha Porto, Chuo Kikuu cha Coimbra na Chuo Kikuu cha Lisbon.

Wajumbe hao pia wametembelea baadhi ya jumuiya za kimataifa kama vile Ofisi za Umoja wa Mataifa katika Vienna na Geneva, Shirika la Kimataifa la Kazi, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, Shirika la Miliki Bunifu la Dunia, Umoja wa Mawasiliano wa Dunia, Baraza la Uchumi la Dunia.

Licha ya hayo, wajumbe wametembelea balozi za China nchini Austria na Ureno na jumbe za China katika mashirika ya kimataifa mjini Vienna. Wamefanya mazungumzo na wahitimu wa BFSU nchini Uswisi, na pia kuanzisha kituo cha mafunzo ya vitendo cha BFSU nchini Ureno.