Tarehe 18 Machi, Balozi wa Cyprus nchini China Bi. Frances Lanitou ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Makamu Mkuu Prof. Zhao Gang amekutana na mgeni huyo na msafara wake. Pande hizo mbili zimefanya mazungumzo juu ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano.
Bi. Lanitou amesifia mafanikio ya BFSU katika kutayarisha wanafunzi. Pia amesema ubalozi wa Cyprus nchini China utahimiza mawasiliano ya wanafunzi na ushirikiano wa ufundishaji na utafiti kati ya nchi hizo mbili.
