Mwanzo > Habari > Content

Balozi wa Ureno Atembelea BFSU

Updated: 2025-03-19

Tarehe 13 Machi, Balozi wa Ureno nchini China Bw. Paulo Nascimento ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amekutana na mgeni huyo na msafara wake. Pande hizo mbili zimefanya mazungumzo juu ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano.

Bw. Nacsimento amesifia mafanikio ya BFSU katika kufundisha na kutayarisha wanafunzi wa Kireno. Pia amesisitiza kwamba ubalozi wa Ureno nchini China utaendelea kuunga mkono maendeleo ya kozi ya Kireno ya BFSU na kuhimiza mawasiliano ya utamaduni kati ya nchi hizo mbili.


站长统计