Tarehe 26 Februari, Kitivo cha Biashara ya Kimataifa cha BFSU kimepokea barua rasmi kutoka Jumuiya ya Wahitimu wa Kitivo cha Biashara ya Uingereza(BGA). Barua hii imetoa pongezi kwa Kitivo hicho ambacho kimetunukiwa ithibati ya BGA kwa miaka mitatu.
Ithibati inayotolewa na BGA ni miongoni mwa ithibati tatu zenye kiwango cha juu duniani. Ithibati hiyo imeonesha kwamba BFSU imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa Kitivo hicho cha Biashara ya Kimataifa.
