Tarehe 30 Januari, sherehe ya mwaka mpya ya walimu wa kigeni imefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU. Walimu wote wa kigeni wa BFSU na familia zao, wawakilishi wa walimu na wanafunzi zaidi ya 100 wameshiriki sherehe hiyo. Makamu Mkuu Prof. Zhao Gang ametoa risala kwenye sherehe na kuwatakia heri na fanaka.
Walimu wanne waliofundisha zaidi ya miaka 10 katika BFSU wametunukiwa tuzo. Prof. Charassri Jiraphas wa Kitivo cha Masomo ya Asia, Prof. Wang Dehong na Dr. Chun Ethan Forbes wa Kitivo cha Biashara ya Kimataifa, Dr. Matsuda Takahiro wa Kitivo cha Lugha na Utamaduni wa Kichina wametoa hotuba.
Zaidi ya hayo, walimu na wanafunzi wameandaa burudani mbalimbali na kusherekekea mwaka mpya kwa pamoja.
