Mnamo tarehe 17 hadi 18 Desemba, Kongamano la Nane la Kiswahili la Kimataifa limefanyika Pemba, Zanzibar. Zaidi ya wasomi 150 wanaotoka nchi 10 wameshiriki kwenye Kongamano hilo.
Mwanafunzi wa shahada ya uzamili wa BFSU Bw. Qin Zulong ameshiriki Kongamano hilo akiwasilisha ripoti inayochambua makosa ya kisarufi ya wanafunzi wa Kiswahili wa China katika mchakato wa upatanishi.
Qin amezungumza na wasomi mashuhuri mbalimbali wa Kiswahili na kupewa vitabu na Prof. Kahigi wa UDSM na Dr. Ponera wa UDOM. Ziara hiyo imeimarisha mawasiliano kati ya idara ya Kiswahili ya BFSU na taasisi za Kiswahili za kimataifa.