Kuanzia tarehe 14 hadi 23 Desemba, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian ameongoza ujumbe kutembelea Saudi Arabia, Misri na Algeria. Wajumbe hawa wametembelea Chuo Kikuu cha Mwana wa Mfalme Sultan na Chuo Kikuu cha Binti wa Mfalme Nourah Bint Abdulrahman nchini Saudi Arabia, Chuo Kikuu cha Ain Shams, Chuo Kikuu cha Badr nchini Misri na Chuo Kikuu cha Algiers III nchini Algeria kwa ajili ya kuzidisha mawasiliano kati ya vyuo vikuu.
Wajumbe hawa pia wametembelea taasisi mbalimbali zikiwemo Kituo cha Utafiti wa Ghuba na Kituo cha Mawasiliano na Utafiti wa Ujuzi nchini Saudi Arabia, Kamati ya Tafsiri ya Baraza la Utamaduni la Misri na Jumuiya ya Urafiki wa Algeria-China ili kuimarisha ushirikiano kati ya BFSU na serikali, jumuiya na taasisi.
Wametembelea balozi za China nchini Saudi Arabia, Misri na Algeria pamoja na wakala wa Huawei nchini Saudi Arabia na kuwatembelea wahitimu na wanafunzi wa BFSU wanaofanya kazi na kusoma katika nchi hizo tatu.