Mwanzo > Habari > Content

Kongamano la Taasisi za Confucius za BFSU Lafanyika

Updated: 2024-11-25

Tarehe 18 Novemba, Kongamano la Taasisi za Confucius za BFSU limefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU. Kongamano hilo lenye kaulimbiu ya Kufunzana na Kuandika Sura Mpya ya Maendeleo ya Taasisi za Confucius kwa Pamoja limelenga kuimarisha mawasiliano na kuhimiza maendeleo ya daraja la juu ya taasisi hizo. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian ameshiriki kwenye ufunguzi wa Kongamano.

Wakurugenzi na viongozi wa Taasisi (Madarasa) za Confucius 22 za BFSU wamehudhuria kwenye ufunguzi, na wawakilishi hao wamezungumza vya kutosha katika majukwaa ya Utayarishaji wa Walimu, Upanuzi wa Ushirikiano na Maandalizi ya Miradi Maalum.