Kuanzia tarehe 15 hadi 17 Novemba, Mkutano wa Kimataifa wa Lugha ya Kichina 2024 umefanyika jijini Beijing. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Mawasiliano na Mwingiliano, Urithi na Ubunifu”. Zaidi ya wasomi, wataalamu, mabalozi na wawakilishi 2,000 wa asasi za elimu, vyuo vikuu, makampuni na mashirika ya kimataifa kutoka nchi na kanda zaidi ya 160 wamehudhuria mkutano huo. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian, Makamu Mkuu Prof. Liu Xinlu wamealikwa kushiriki mkutano. Katika “Kongamalo la Uanzishaji wa Taasisi za Confucius Miaka 20”, Prof. Jia Wenjian ametoa hotuba yenye mada ya “Kufunzana na Kuandika Sura Mpya ya Maendeleo ya Taasisi za Confucius kwa Pamoja”.